Kuhusu Programu ya Semina Elekezi za IKHLA

Ibn Khaldun Learning Academy (IKHLA), kwa kushirikiana na washirika wake wakuu kama Wete Institute of Academic Research and Consultancy (WIARC) na Wete Charity Organization (WECO), pamoja na wadau wengine wa elimu katika Mji wa Wete, imeanzisha na kuendesha Programu ya Semina Elekezi kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita wanaomaliza masomo na wale wanaomaliza vyuo vikuu. Semina hizi ni sehemu ya juhudi za IKHLA katika kuandaa vijana kwa maisha ya chuo, maisha ya kitaaluma, na uongozi wa kijamii, kwa kuwapa maarifa, motisha, na mbinu za kujitegemea na kuchangia maendeleo ya jamii.

Malengo ya Programu

  1. Malengo ya Semina Elekezi Kuwasaidia wanafunzi waliomaliza Kidato cha Sita kujua hatua muhimu za kujiunga na vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu.
  2. Kutoa mwongozo kwa wahitimu wa vyuo vikuu juu ya mbinu za kuendeleza taaluma zao au kujiajiri.
  3. Kuwaandaa vijana kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa jamii yao kupitia miradi ya maendeleo na huduma za kijamii.
  4. Kukuza fikra za ubunifu, ujasiriamali, na majukumu ya kijamii kwa kizazi kijacho cha viongozi na wataalamu.

Yaliyojumuishwa katika Semina

  1. Mafunzo ya Maandalizi ya Chuo: Mchakato wa maombi ya vyuo, ushauri wa kozi, na mbinu bora za kusoma katika elimu ya juu.
  2. Maendeleo ya Kitaaluma: Kuandaa CV, maandalizi ya mahojiano ya kazi, na ujuzi wa kujiuza kitaaluma
  3. Ujasiriamali na Kujitegemea: Njia za kuanzisha miradi midogo, kutafuta fursa za biashara, na umuhimu wa kujiajiri.
  4. Uongozi na Huduma kwa Jamii: Kukuza moyo wa kujitolea, ushiriki wa kijamii, na majukumu ya kijamii baada ya masomo.
  5. Motisha na Uhamasishaji: Ushuhuda kutoka kwa watu waliopitia safari kama yao, wakitoa hamasa na mwanga wa matumaini.

Wanaonufaika

  1. Wanafunzi waliomaliza Kidato cha Sita wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu.
  2. Wahitimu wa vyuo vikuu wanaotarajia kuingia katika soko la ajira au kuanzisha shughuli binafsi.
  3. Vijana wa Mji wa Wete na maeneo jirani wanaotafuta maarifa zaidi ya kuwaandaa kwa hatua inayofuata maishani.

Wadau Washirika

Programu hii inatekelezwa kwa mafanikio makubwa kupitia ushirikiano wa karibu na:

  1. WIARC (Wete International Academic and Research Center)
  2. WECO (Wete Charity Organization)
  3. WTaasisi za elimu za ndani na nje
  4. Wadau wa maendeleo ya vijana na elimu

Ripoti

Bonyeza hapa kupakua ripoti ya Semina Elekezi